Find out what I'm doing, Follow Me :)

Monday 15 December 2014

ZIJUE SIRI ZA WAJASIRIAMALI MATAJIRI.

Wakati unafikiria kuhusu watu ambao ni mamilionea au mabilionea unapata picha/taswira gani akilini mwako?

Nadhani wengi wenu mnahisi ni wale ambao wanatembea na ndege binafsi, wanaoenda kufanya shopping nchi za ugenini, na wanaotumia pesa zao kula bata. 
Lakini ukweli ni kwamba mamilionea/bilionea wengi huishi maisha ya kawaida sana, hufanya kazi zao kwa muda kamili bila kuwaza kula na isitoshe hata hufanya shoppings zao katika sehemu za kawaida kama tunazofanya sisi wengine.

Kikubwa ni kwamba vitu vinavyowapa motisha matajiri sio 'Material things' bali ni maamuzi au machaguo ambayo fedha zinaweza kuwaletea.

Matajiri hawapo katika kupata more material stuffs, ila wapo katika kupata uhuru wa kifedha utakaowawezesha kufanya maamuzi yoyote watakayotaka kuyafanya.
Kwao utajiri una maanisha kuacha kazi usiyoipenda na kufanya kile unachokipenda hata kama ni kidogo.

Unataka kuwa tajiri mkubwa Tanzania kama Said Salim Bakhresa, Mohamed Dewji, Rostam Aziz, Nazir Mustafa Karamagi, Reginald Mengi, Yusuf Manji, nk basi zifahamu njia ambazo wengi wanazitumia katika kuendelea kuwa wajasiriamali matajiri wakubwa Tanzania na duniani.

Hizi ni SIRI tano (5) ambazo matajiri wengi walizitumia mpaka kufikia hapo walipo:

1. USIPOTEZE MWELEKEO WA UNAPOTAKA KUFIKA/KWENDA.

Kutaka kuwa tajiri ni moja ya hatua ya kwanza ya muhimu. Lakini kikwazo kikubwa kinachowafanya watu wengi washindwe kuwa matajiri ni ile HOFU waliyonayo.

Watu wengi wanaogopa kuTHINK BIG, wengi wanaogopa KUTHUBUTU ndio maana wanapoteza muelekeo wa ndoto zao za kuwa matajiri wakubwa duniani.

Hawatambui kuwa ili kuwa tajiri ni lazima upitie misukosuko mingi, ni lazima ufeli ili uweze kujifunza kutokana na makosa yako.

Ili uweze kutimiza malengo yako ya kuwa tajiri ni lazima ujiamini na uamini kuwa ipo siku utafanikiwa, kamwe usipoteze muelekeo wa pale unapotaka kuwepo au kufika maishani mwako.

2. JIELIMISHE WEWE MWENYEWE:

Kujielimisha haimaanishi ukajiandikishe kuingia chuo, usome, ukafanye mitihani kisha uje kuwa tajiri lahasha.

Tambua kuwa watu wote ambao ni matajiri wakubwa duniani hawakufanikiwa kwa elimu yao ya darasani.

Ili uweze kuwa tajiri mkubwa ni lazima uijue kwa kina ELIMU YA UHURU WA KIFEDHA.
Na kawaida elimu hii haifundishwi madarasani, ndio maana watu wanamaliza kusoma mpaka phd lakini hawana uhuru wa kifedha.

Unachotakiwa kukifanya ni kusoma vitabu vitakavyokufungua mawazo yako juu ya njia zakuifanya pesa/hela/fedha zikufanyie wewe kazi na sio wewe kuifanyia kazi pesa, ujifunze toka kwa watu waliofanikiwa ili uweze kuwa na elimu ya kutosha itakayokusaidia kufikia malengo yako ya kuwa tajiri. Uondokane na hofu ya KUWEKEZA, ujue namna ya kuifanya pesa izae na kuongezeka kila siku ili ije kusaidia vizazi vyako vyote.

3. FANYA KITU UNACHOKIPENDA.

Siku zote 'Passion pays off.' Hicho unachotaka kukifanya au unachokifanya kama unakifanya kwa moyo wako wote lazima kitakulipa tu, iwe leo, kesho au hata kama ni baada ya mwaka kitakulipa tu.

Tatizo letu kubwa wa Africa tunaamini sana katika kuajiriwa ndio maana tunaua vipaji tulivyozaliwa navyo na kukimbilia kufanya kazi ambazo hatuzipendi ili mradi tu mwisho wa mwezi tupate kipato na hii yote inatokana na HOFU. Hofu ya kutokujua tutapata wapi pesa zakulipia kodi ya nyumba, fremu ya biashara unayotaka kupangisha, kulipa ada za watoto, nk na ndio maana kuwa matajiri ni kazi kubwa kweli kweli.

Ukiacha kufikiria kuhusu 'pay check' na kufikiria zaidi kufanya kile unachokipenda, utakuja kugundua kuwa una vipaji vingi sana ambavyo Mungu wako amekujalia ambavyo ukianza kweli kuvifanyia kazi basi vitakunufaisha na kukufikisha mbali.

Ukiweza kugundua kuwa unachokifanya hukipendi na kuachana nacho na kuamua kufanya kile unachokipenda kwa dhati toka ndani ya moyo wako basi hakika utakuwa tajiri mkubwa sana duniani.

Wengi wana vipaji kama vile vya Uandishi na utunzi vitabu, utangazaji hodari kama millardayo, kipaji cha kupiga picha, kipaji cha kuimba kama Barnaba, Ben pol na wengineo, kipaji cha kuwa kiongozi kama Zitto Kabwe, nk lakini hatuvitumii vipaji tulivyonavyo kama moja ya wazo la biashara, matokeo yake tunakimbilia kuajiriwa kwenye shirika la ndege au benki ili mradi tu na wewe uonekane unafanya kazi katika ofisi fulani yenye hadhi, kumbe hatujui tunawauzia wengine ujuzi na muda wetu katika kuwanufaisha wao na ndio maana wao wataendelea kuwa matajiri.

Badilika, zinduka, acha kufikiria kuhusu 'pay check' yako na anza kufikiria ni kipaji gani au kitu gani ulicho na passion nacho na ukifanye kwa moyo.

4. USIOGOPE KUCHUKUA 'RISKS':

Je, una ujasiri wakuchukua (calculative) risks?
Wengi wetu tunapenda kuwa matajiri lakini hatuna GUTS OF TAKING CALCULATIVE RISKS.

Wengi tunaogopa kuwa RISK TAKERS na ndio maana ni ngumu kuwa matajiri.
Waliofanikiwa wote ni wale ambao walikuwa na UJASIRI wakukabiliana na RISKS zozote zitakazojitokeza.

Ukitaka kuwa tajiri ni lazima ukubali kuwa RISK TAKER, usiwe muoga wa kupata hasara, kuogopa kujaribu au kuthubutu kisa unaogopa biashara itakufa.
Matajiri siku zote ni wajanja ndio maana huamua kuwekeza pale tu ambapo wameshafanya 'Calculative risks' na kuona sawa kumbe nitakachokipata ni zaidi ya nitakachokikosa.

Kama na wewe unapenda uwe tajiri basi anza kujifunza kuwa risk taker, usiogope kushindwa, tambua siku zote haziwezi kuwa za ushindi kwako, ila unaweza zitumia vizuri siku za ushindi ili ziweze kufidia siku zitakazokuwa mbaya au kuporomoka kwa biashara yako.
"NO GUTS, NO GLORY."

5. JIFUNZE KUKUZA AU KUZALISHA FEDHA ZAKO:

Wengi wetu tumejizoesha kuishi kwa mshahara wa mwezi hadi mwezi.
Kama umechoka kuwa mtu wa kusubiria mshahara wako wa mwisho wa mwezi ambao pengine unaweza kuchelewa kuupata, basi njia pekee kubwa ya kwanza ni kuwa na DIFFERENT SOURCES OF INCOME (Kuwa na chanzo cha kipato zaidi ya kimoja.). 

Lakini kuwa na njia ya kipato zaidi ya moja haimaanishi kwamba tayari wewe ni tajiri.
Swali ni je, unaweza kuzalisha na kukuza hizo fedha ulizonazo?

Matajiri wanaendelea kuwa matajiri kwa sababu wakipata pesa hawazikumbatii na kulala nazo chumbani, wala hawazitumii ovyo bali wanajua wapi pakuziwekeza na kuzifanya zizae na kukua kizazi hadi kizazi.

Ndio maana matajiri wengi wakipata pesa huamua kuwekeza kwenye migodi, gesi, Real Estates, Hisa, mafuta, kununua franchise, nk kwa sababu wanajua wakifanya hivi pesa zao zitakua na kuzaa maradufu. Lakini sisi watu wa kawaida tukipata pesa zaidi matatizo ndio yanaongezeka, shoppings zinaongezeka, matumizi yasiyo ya muhimu yanakuwa mengi, mwisho wa simu hela zote zinaisha.

Ukitaka kufanikiwa jifunze kuwa na:
i) Chanzo cha kipato zaidi ya kimoja, na usitegemee mshahara uupatao kazini.
ii) Jifunze KUSEVU pesa. Haijalishi ni kiasi gani unatengeneza, bali ni kiasi gani unachobaki nacho au unachokihifadhi.
iii) Punguza Overspending (jifunze kutofautisha WANTS na NEEDS zako).
iv) Penda kuwekeza fesha zako katika ASSETS.

Nakutakia mafanikio mema katika ubilionea wako.

Imeandaliwa na: EriNoe Business & Management Consultancy (Noel) 

3 comments :

  1. kiukweli ni ushauri mzuri na wenye uwaz kwa mtu anayetaka kuwa au tayare ni mjasilia mali

    ReplyDelete
    Replies

    1. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
      Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
      that will make you rich and famous in the world and have
      power to control people in the high place in the worldwide
      .Are you a business man or woman,artist, political,
      musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
      in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
      instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
      home.any where you choose to live in this world
      BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
      1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
      2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
      3.A Dream House bought in the country of your own choice
      4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
      destination.
      5.One year Golf Membership package
      6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
      Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
      account every month as a member
      9.One Month booked Appointment with Top 5 world
      Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
      If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
      or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

      Delete

  2. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
    Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
    that will make you rich and famous in the world and have
    power to control people in the high place in the worldwide
    .Are you a business man or woman,artist, political,
    musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
    in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
    instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
    home.any where you choose to live in this world
    BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
    1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
    2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
    3.A Dream House bought in the country of your own choice
    4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
    destination.
    5.One year Golf Membership package
    6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
    Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
    account every month as a member
    9.One Month booked Appointment with Top 5 world
    Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
    If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
    or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

    ReplyDelete